Taarifa za uhakika zinasema Kocha Nasraddine Mohamed Nabi naye anasubiri ruhusa (Approval) ya CAF kumuwezesha kukaa kwenye benchi hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

Nabi ambaye msimu uliopita alikaa benchi kwenye mechi 2 dhidi ya Rivers United ana vyeti vya UEFA ‘A’ na UEFA-Pro alizosomea Ubelgiji, lakini taarifa zake zilichelewa kupelekwa CAF.

Nabi Kama Mgunda Tu!!

Taarifa zinasema aliyekua Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga SC Thabit Kandoro wakati anaondolewa kwenye nafasi yake kumpisha Saad Kawemba alikuwa anafanya usajili wa wachezaji na Viongozi wa benchi la ufundi.

Akiwa ameshamaliza wachezaji 7 kuwaingiza kwenye mfumo wa usajili akakumbana na andiko la kuachishwa kazi, akamalizia wachezaji ila benchi la ufundi alikua bado hajaanza kabisa.

Nabi Kama Mgunda Tu!!

Kwahiyo waliochukua nafasi badala yake ni kama walipitiwa wakiamini kila kitu kiko sawa wakaja kukumbushwa na ujumbe kutoka CAF juu ya taarifa za kocha wao.

Habari zaidi zinasema taarifa zake (vyeti) zimeshawasilishwa CAF na wanasubiri Shirikisho hilo la Soka Afrika kuidhinisha tu ili akae benchini kesho.

Nabi Kama Mgunda Tu!!

Hali hii ni kama ambayo inamkuta Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda ambaye na yeye anasubiria idhini ya CAF ili kesho akae benchini pale Jijini Lilongwe kwenye mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets. Mgunda yeye amechlewa kuidhinishwa kwakuwa vyeti vyake vimechelewa kuwasilishwa kwakuwa ni kocha mpya.

Ameandika Mchambuzi wa Efm Jemedari Said Kazumari “The Voice of Voiceless”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa