Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda, amesema kuwa atamtumia kiungo wake mgumu kwenye mechi za ligi kwa kuwa adhabu yake itakuwa imegota mwisho.

Kanoute alionyeshwa kadi mbili za njano mbele ya Coastal Union, Desemba 3,2022 ubao uliposoma Coastal Union 0-3 Simba ile ya kwanza alionyeshwa dakika ya 40 na ya pili alionyeshwa dakika ya 90.

Sadio Kanoute Kuiwahi Geita Gold Fc

Mgunda amesema:-“ Kenoute atakosa mchezo mmoja ile ni adhabu ambayo ameipata na ukweli ni kwamba ni mchezaji wangu muhimu tutamkosa kwenye mchezo mmoja.
“Tutamkosa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hivyo nina amini kwamba atarejea kwenye mechi zetu za ligi kuendelea kutimiza majukumu yake.

Sadio Kanoute Kuiwahi Geita Gold Fc

“Tumemaliza mzunguko wa kwanza na sasa hesabu ni kwenye mzunguko wetu wa pili unaona vijana wanacheza kwa kujituma na uwepo wa mashabiki unatufanya tunaendelea kupata matokeo,” alisema Mgunda.

Ataukosa mchezo dhidi ya Eagle ambao ni wa Kombe la Shirikisho raundi ya Pili unaotarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 9/11 ataibuka kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold, Desemba 18, Uwanja wa Nyankumbu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa