Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Salim Abdallah Try Again amekanusha taarifa za klabu hiyo kudaiwa posho na wachezaji wao kama ambavyo habari zinasambaa.
Salim Try Again amesema taarifa ambazo zinasambaa kua klabu yao inadaiwa posho na wachezaji klabuni hapo sio za kweli na klabu hiyo ni moja ya klabu zinazolipa posho nzuri zaidi nchini.Kiongozi huyo wa Simba ameeleza pia klabu ya Simba iliwaahidi wachezaji kiasi cha shilingi milioni 500 kama wangeshinda mchezo wa kwanza kwenye michuano ya African Football League, Lakini vilevile wakatoa ahadi ya bilioni moja kama wangeshinda ugenini jambo ambalo halikufanikiwa.
Klabu ya Simba imekua ikituhumiwa kutowalipa wachezaji wake posho na wanadai posho kwa klabu hiyo za zaidi ya mchezo mmoja, Lakini kiongozi huyo akifanya mahojiano leo na wanahabari wamekanusha taarifa hizo.Mwenyekiti Salim Try Again pia amegusia suala la usajili na kusema wataingia sokoni mwezi Januari na kusajili wachezaji wenye ubora, Lakini akitoa angalizo pia wachezaji waliopo kama watashindwa kujituma wataachwa.