Klabu ya Manchester United inaelezwa kupanga kumuuza kiungo wa kimataifa wa Brazil klabuni hapo Carlos Casemiro baada ya kudumu kwa msimu mmoja tu klabuni hapo.

Casemiro alijiunga na Manchester United msimu ulimalizika akitokea klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ambapo amedumu ndani ya timu hiyo kwa msimu mmoja akioneshe ubora mkubwa.manchester unitedKiungo huyo wa kimataifa wa Brazil alikua na ubora mkubwa sana msimu uliomalizika ambapo ndio alijiunga klabuni hapo, Lakini msimu huu ubora wake umeonekana kuporomoka lakini pia akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Sir Jim Ratcliff ndio anaelezwa kutaka kumuuza kiungo huyo pale ambapo atafanikiwa kumaliza mchakato wa kununua hisa zake 25% ambazo atakua anamiliki ndani ya klabu hiyo.manchester unitedBosi huyo ndio anaelezwa kua na mipango ya kumuuza Casemiro kwa lengo la kuanza kutengeneza mradi mpya ndani ya klabu hiyo, Kwani anaamini klabu itapata pesa nzuri kwa kumuuza mchezaji huyo na baada ya hapo watasajili wachezaji wadogo kwajili ya mipango ya muda mrefu ndani ya Manchester United.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa