Aliekua kipa wa klabu ya Mtibwa Sugar Farouk Shikalo ametimka ndani ya walima miwa kutoka mkoani Morogoro katika klabu ya Mtibwa Sugar.

Golikipa huyo amesitisha mkataba wake na klabu hiyo na kuamua kurudi nchini Kenya ambapo ndiyo nyumbani kwao haswa. Golikipa huyo amesitisha mkataba na klabu hiyo huku taarifa rasmi zikiwa bado hazijaeleza chanzo cha kuvunja mkataba wake na Mtibwa Sugar.shikaloShikalo anaeleza kua umamuzi huo aliuchukua tangu siku ambayo klabu yake ya Mtibwa Sugar ilipoteza kwa mabao manne kwa moja dhidi ya klabu ya Azam Fc katika mchezo uliopigwa katika dimba la Manungu Complex mkoani Morogoro.

Golikipa Shikalo ambaye ameidakia klabu ya Yanga kwa misimu miwili kabla ya kutimkia katika klabu ya KMC ambapo alidumu kwa msimu na kuhamia kunako klabu ya Mtibwa Sugar msimu huu kabla ya kuamua kusitisha mkataba na walima miwa kwa sababu ambazo hazijaekwa wazi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa