Baada ya ushindi mwembamba uliopita dhidi ya Ihefu, Simba inatarajia kumualika Namungo Fc katika mchezo wake wa 11 kwenye Ligi ambapo mchezo huo utapigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 jioni.

 

Simba Kusaka Pointi 3 Kesho Dhidi ya Namungo

Simba ilipata ushindi huo huku ikigubikwa na wachezaji majeruhi takribani watatu, Israel Mwenda, Peter Banda na Sakho aliyeumia mchezo uliopita huku pia kiungo wao Cloutus Chama ukiwa huu ni mchezo wake wa mwisho kuwa nje.

Chama alifungiwa na TFF kucheza michezo mitatu ukiwepo mchezo wa Singida Big Stars, Ihefu na huu wa leo dhidi ya Namungo, huku Wekundu wa Msimbazi wakipata shida kwenye eneo la Chama.

Namungo baada ya kucheza michezo 10 kwenye ligi wapo nafasi ya 6, wakiwa na ushindi mara nne, sare tatu na kupoteza mara 3 pointi zao 15 kibindoni. Vijana wa Mgunda nafasi ya 3 kupoteza mara moja na ushindi mara 6 pointi 21 hadi sasa.

Simba Kusaka Pointi 3 Kesho Dhidi ya Namungo

Mechi nne za mwisho za Ligi Simba kashinda tatu, huku wakienda sare mara moja, Na Namungo tangu apande ligi msimu wa 2019 hajawahi kupata pointi 3 kwa mnyama.

Namungo wana mchezaji wao ambaye ndiye kinara wa mabao Ligi kuu Reliants Lusajo akipachika mabao 6 huku Mosses Phiri akiwa na mabao 5 pekee.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa