Klabu ya soka ya Simba inatarajia kutangaza kocha wa Viungo leo hii baada ya kukaa muda kidogo bila ya kua na kocha wa viungo klabuni hapo, Hivo leo klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi imepanga kutangaza kocha mpya wa viungo leo.

Klabu hiyo inatarajia kumtangaza kocha huyo siku ya leo na inasemekana kocha huyo ni raia wa Morocco na ametoka kufundisha klabu ya umoja wa falme za kiarabu akifahamika kama Zakaria Chlouha.simbaKlabu ya Simba imekosa kipa wa makipa na kocha wa viungo kwasasa jambo ambalo halijawapendeza baadhi ya wadau wa klabu hiyo na kuona kama sio hadhi ya klabu hiyo kukaa bila kua na kocha wa mazoezi na kocha wa magolikipa.

Klabu hiyo ambayo imebakiwa na kocha Mgunda tu baada ya kocha Suleiman Matola kwenda masomoni kuongeza elimu hivo klabu hiyo inahitaji kuongeza wigo kwenye benchi lake la Ufundi.

Inaelezwa kocha ambaye anatarajia kutangazwa ndani ya klabu ya Simba ni kocha mwenye uwezo wa kufanya majukumu mawili kwa wakati mmoja. Kocha Zakaria Chlouha ana uwezo wa kusimama kama kocha wa makipa pia kama kocha wa viungo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa