Mchezaji wa Mancheter City na timu ya Taifa ya Ujerumani Ilkay Gundogan ambaye anacheza kama kiungo wa timu hiyo, mkataba wake unamalizika mwezi Juni katika timu hiyo.
Na Gundogan amesema kuwa msimu wa joto wa 2023 bado anahisi kuwa mbali sana na kwasasa amepumzika na hata haijulikani ni nini kitatokea kwa kocha wao huyo Guardiola ambaye amewapa mafanikio klabuni hapo.
Aliongezea kwa kusema kuwa; “Ninajisikia vizuri sana hapa Manchester na nina furaha.”
Pia aliulizwa kuhusu kuhamia katika klabu ya Liverpool na akajibu kuwa kwasasa hapana bado yupo kwa Pep Guardiola.
Mancester City wametoka kupoteza mchezo wao wa mwisho kabla ya kuelekea Kombe la Dunia wakiwa nyumbani baada ya kutunguliwa na Brentford kwa mbao 2-1 huku Ivan Toney akiwaadhibu katika dakika za nyongeza za mcheo huo.
Gundogan ataenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia akiiwakilisha Ujerumani ambao walichukua Kombe hilo mwaka 2014, kabla ya mabingwa watetezi Ufaransa kubeba taji hilo mwaka 2018.