Baada ya kulazimishwa sare nyumbani kwake mchezo uliopita, Geita Gold kesho inatarajiwa kuwa wageni wa Tanzania Prison katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya majira ya saa 10:00 jioni.
Tanzania Prison yupo nafasi ya 9, baada ya kucheza michezo 11, ushindi mara tatu, sare tano, kupoteza mara tatu na pointi zao 14 kibindoni, wakati Geita wao wamecheza michezo 11, nafasi ya 10 kushinda mara tatu, sare tano, na kupoteza mara tatu pointi 14.
Mechi ya mwisho ya Prison alipoteza, huku Geita akijipatia sare kinachowatofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Wote wakiwa na pointi sawa kwenye Ligi kuu wanakutana ili kila mmoja aondoke na pointi tatu na mwenyeji akisema kuwa amejiandaa kuondoka na pointi 3. Je Mgeni anweza kukubali kuachia pointi hizo baada ya mechi ya mwisho kuambulia pointi moja?