Staa wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo anaamini klabu hiyo haiwezi kufika kwenye viwango vya juu siku za hivi karibuni kutokana na mambo ambayo yanaendelea ndani ya klabu hiyo.

Staa huyo ambaye amezungumza mambo mengi siku kadhaa nyuma amezungumza mambo mengi kuhusiana na klabu hiyo baada ya kufanya mahojiano na mtangazaji nguli nchini Uingereza Piers Morgan.ronaldo, Ronaldo: Siioni United kwenye Kiwango cha Juu Karibuni, MeridianbetRonaldo anaamini klabu hiyo haiwezi kwenye kiwango cha juu kwa miaka miwili au mitatu ijayo kwasababu kuna vitu vinayoendelea ndani ya klabu ambavyo haviwezi kuisaidia timu hiyo kufika kwenye kiwango cha juu.

Ndani ya mahojiano hayo gwiji huyo pia alieleza kua anataka klabu hiyo ifanye vizuri na kurudi kwenye ubora wake ndo maana ameamua kusema ukweli na ili kuweza kuisaidia klabu hiyo na mashabiki wanastahili kusikia ukweli.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amezungumza mambo mengi ya hovyo yanayoendelea ndani ya klabu hiyo ambapo imeweza kugawanya mashabiki wengine wakiamini yuko sahihi na wengine wakiona hayupo sahihi.ronaldo, Ronaldo: Siioni United kwenye Kiwango cha Juu Karibuni, MeridianbetRonaldo yeye anaona klabu hiyo inahitaji kua na misingi mizuri kutoka ngazi ya juu ya klabu na miundombinu akizitaja klabu kama Man City,Liverpool, na Arsenal kwamba ni klabu ambazo kwasasa ziko juu na United inapaswa kufata utaratibu wanaotumia vilabu hivo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa