UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ipo wazi kwamba mchezo uliopita Simba ilikuwa ugenini ilivuna pointi tatu dhidi ya Geita Gold kwa bao la Babacarr Sarr dakika ya 81 kwenye mchezo huo akitumia pasi ya Kibu Dennis.
Februari 15 inatarajiwa kucheza na JKT Tanzania mchezo wa kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kuwa ni mechi 14 Simba imecheza na pointi 33 kibindoni.Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo kwenye ligi watapambana kupata matokeo.
“Ugumu ni mkubwa na ushindani upo wapinzani wetu tunawaheshimu lakini tutaingia kwenye mchezo huo kwa tahahadhari kupata pointi tatu,”.
Mara ya mwisho JKT Tanzania kucheza dhidi ya Simba SC kwenye ligi kuu ilikuwa Machi 1, 2021 Uwanja wa Mkapa na Simba ilikomba pointi tatu.
Mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi Februari 15, 2024 saa 10:00 jioni utachezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.