Klabu ya Simba imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la Azam Federation baada ya kupata ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya klabu ya African Sports kutoka mkoani Tanga.
Simba sasa imefanikiwa kufuzu hatua inayofuata baada ya ushindi mnono wa leo wa mabao manne kwa bila dhidi ya African Sports, Mabao ya Wekundu wa Msimbazi yaliwekwa kimiani na Jean Baleke,Kennesy Juma, Mohamed Mussa, kabla ya Jimmyson Mwinuke kupigilia msimari wa bao la nne na kuhiimisha karamu hiyo ya mabao.Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa akuonesha kiwango kizuri dhidi ya African Sports inayoshiriki ligi daraja la pili, Huku wachezaji wengi ambao wamekua hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza klabu wakionekana kupata muda mwingi wa kucheza leo hii.
Simba sasa wanajiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa siku ya tarehe 7 Jumanne kwenye dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya Vipers kutoka nchini Uganda, Hivo kupitia ushindi wa leo inaongeza ari kuelekea mchezo huo muhimu zaidi kwao.Klabu ya Simba wamebakiza michezo miwili nyumbani kwajili ya kutetea nafasi yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika kama yalivyo malengo yao, Hivo mchezo dhidi ya Vipers ni muhimu sana kwao huku wakimaliza na klabu ya Horoya pia kwenye dimba la Benjamin Mkapa na wakifanikiwa kubeba alama sita kwenye uwanja wa nyumbani basi ni wazi wanaweza kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kwenda robo fainali.