Klabu ya Real Madrid imethibitika wanamfukuzia winga hatari wa klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Khvicha Kvaratskhelia kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Georgia.
Real Madrid wanaelezwa bado wanataka kuiboresha klabu hiyo hasa kwenye upande wao wa pembeni baada ya kumkosa nyota wa klabu ya PSG raia wa kimatifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, Hivo Kvaratskhelia ameingia kwenye rada za klabu hiyo kuelekea dirisha kubwa la mwezi Juni.Real Madrid wanahitaji kupata winga mwenye kiwango cha dunia ambaye atashirikiana na Vinicius Jr klabuni hapo ili kuweza kuwafanya mabingwa hao watetezi barani ulaya kuendelea kua bora na kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ambayo wmaekua wakishiriki.
Khvicha Kvaratskhelia amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Napoli tangu ajiunge klabuni hapo akitokea klabu ya Dinamo Batumi kutoka nchini Urusi mwaka 2022.Mchezaji Kvaratskhelia amekua na ushirikiano mzuri pamoja na mshambuliaji Victor Osimhen wakifanikiwa kutengeneza safu kali ya ushambuliaji ndani ya klabu ya Napoli, Huku wakiifanya klabu hiyo kua tishio zaidi barani ulaya na kufanya vilabu mbalimbali kuvutiwa na winga huyo.