Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United aliopo kwenye kiwango bora kabisa Marcus Rashford ametajwa kuwania tuzo ya mcheza bora wa mwezi Debuari ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

Marcus Rashford ataungana na wachezaji wenzake kama Kelechi Iheanacho kutoka Leicester, Solomon kutoka Fulham, Benard Leno kutoka Fulham, Emerson Royal kutoka Tottenham, pamoja na Olie Watkins kutoka klabu ya Aston Villa ambao wamekua kwenye kiwango bora ndani ya mwezi Febuari.marcus RashfordWachezaji hao waliotajwa wameonekana kufanya vizuri ndani ya mwezi Febuari ndani ya ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa, Huku orodha hiyo ikiwa imetolewa mapema mchana wa leo na tuzo hiyo ikitarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kura kupigwa na mashabiki ili kutambua ni mchezaji gani ataibuka kinara.

Marcus Rashford anaonekana kua na takwimu nzuri kuwazidi wenzake wote kwani mchezaji huyo kwenye michezo minne aliyoitumikia klabu yake ya Manchester United ndani ya mwezi Febuari amefanikiwa kufunga katika kila mchezo wa ligi hiyo, Lakini pia amefunga magoli matano ikiwa ni idadi kubwa kuliko michezo aliyocheza.marcus RashfordMshambuliaji Marcus Rashford anaweza kuandika rekodi nyingine ya kushinda mchezaji bora wa mwezi mara tatu ndani ya msimu mmoja, Kwani mchezaji huyo tayari ameshafanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ndani ya mwezi Septemba, na Januari mwaka huu hivo kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo tena na mpaka sasa anaongoza kwa takwimu inamuweka kwenye mazingira mazuri ya kushinda tuzo hiyo tena.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa