Simba Yakubali Yaishe, Lameck Lawi Anaenda Ulaya

MCHEZAJI Lameck Lawi na Uongozi wa Coastal Union wapo kwenye mchakato wa mwisho wa kukamilisha vibali vya Beki huyo kusafiri kuelekea nchini Ubelgiji ambapo inatarajiwa atajiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Bado haijawekwa wazi ila vyanzo vyangu kutoka Ubelgiji ni kuwa anaelekea K.A.A GENT endapo atafuzu vipimo vya afya.

Wagosi wa Kaya inaaminika kuwa watakunja kiasi cha EURO 100,000 kwenye biashara hiyo ikiwa ni sawa na MILLION 287 za Kitanzania huku wakiweka kifungu cha onward resale, ikiwa na maana watakunja pesa nyingine endapo Gent watafanya biashara nyingine ya kuuza mchezaji huyo.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Afisa habari wa Coastal Union akitolea ufafanuzi hatma ya Lameck Lawi, beki ambaye Simba imemtambulisha kama mchezaji wao alisema kwamba Beki huyo yupo Tanga na wenzake kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya.

“Tangu jana tumeanza maandalizi yetu kuelekea msimu ujao, sisi tuliweka wazi Lameck Lawi ataripoti Coastal Union atajianda na wenzake na ataenda CECAFA tukawaambia wana Coastal wasiwe na wasi , nadhani watu ni mashahidi Lawi yupo Tanga”

“Tangu walipokuwa hawajakamilisha taratibu sisi tulitoa taarifa na fedha ikarudishwa kila kitu kikawa kimeishia pale , kilichobaki kilikuwa ni kila mmoja kuendelea na maisha yake”

“Tulishamaliza issue ya Lawi kwa kuwafahamisha wenzetu kwamba hili dili halipo , ina maana kila mtu aendelee na maisha yake “

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe