Simba Yawasili Bongo

Klabu ya soka ya Simba imewasili nchini Tanzania mapema mchana wa leo baada ya kumaliza kambi fupi ya siiku saba waliyoweka nchini Dubai.

Klabu ya Simba imewasili nchini ikiwa na kocha wake mpya ambaye atakwenda kuisimamia klabu hiyo katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya NBC. Wekundu wa msimbazi baada ya kumaliza likizo fupi nchini Dubai sasa wanarejea nchini kwajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali ambayo wanashiriki.simbaKlabu ya Simba itakua haina muda wa kupumzika baada ya kutoka kwenye mapumziko mafupi nchini Dubai, Klabu hiyo inatarajia kukipiga na klabu ya Mbeya City katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kocha mpya wa klabu hiyo Roberto Oliviera maarufu kama Robertinho atakua anaisimamia klabu hiyo mechi ya kwanza ya kiushindani klabu hiyo hapo kesho, Lakini wakati huohuo atapata fursa ya kuwaona wachezaji wapya waliosajiiliwa klabu hapo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.simbaKlabu hiyo pia imefanikiwa kufanya maboresho kwenye kikosi chake kwenye dirisha dogo ambalo limefungwa siku moja iliyopita, Wachezaji kama Saidoo Ntibazonkiza, Ismael Sawadogo, Jean Baleke, pamoja Mohamed Mussa ni baadhi ya wachezaji walioimarisha kikosi cha Simba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.