STRAIKA LA MABAO YANGA LATUMA SALAMU KWA BALEKE

STRAIKA wa Yanga aliyefunga bao lililowapeleka kwenye makundi la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, Clement (Walid) Mzize ametuma salamu nzito kwa kinara wa mabao wa sasa ligi kuu kutoka Simba Jean Baleke.

Mzize ambaye hakutaja moja kwa moja kuwa salamu hizo ni za Baleke, alisema kuwa anataka kukumbukwa kwa kufunga mabao mengi kwenye kila msimu na kazi hiyo anataka kuianza msimu huu.YANGA Mshambuliaji huyo wa Yanga alikazia kuwa hataki kutajwa kuwa alitoa assit nyingi ndani ya msimu mmoja, yeye anataka kukumbukwa kwa kuwa mchezaji ambaye alifunga mabao mengi kwenye msimu mmoja na kwa malengo makubwa aliyonayo atafikia kwenye hatua hiyo.

Hadi sasa Baleke ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mabao matano kwenye mechi tatu, huku Mzize akiwa anajitafuta kwenye ligi, huku kwenye kimataifa akiwa ameshaweka chuma mbili.

“Watu waliona kazi yangu ambayo nilifanya msimu uliopita. Niliaminiwa na nikafanya kazi, msimu huu nina malengo makubwa sana, sitaki kukumbukwa kwa assit nyingi ndani ya Yanga.YANGA“Nataka kukumbukwa kwa kuwa mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja,” alisema Mzize.

Acha ujumbe