KESHO Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Yanga watacheza mechi ya marudiano dhidi ya Al Merreikh kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa msimu huu klabu ya Yanga haijapoteza Mchezo wowote katika Uwanja wa Azam Complex kwa michezo ya CAFCL na hata NBC, takwimu zao ni za kupendeza sana.Yanga Sc wameshacheza michezo 6 katika dimba hilo huku wakiwa wameshafunga mabao 40.
Takwimu za Yanga Chamazi kwa Msimu huu
▪Michezo 6 (Nbc 3, Cafcl 3)
▪Mashuti 40
▪Wametengeneza nafasi 58
▪Wakifunga magoli 18 + 2 ya Ya mbali (Jumla 20),
▪Clean Sheet 5Yanga Sc wameruhusu kufungwa goli 1 dhidi ya Asas ya Djibout ambapo walifungwa kwa mkwaju wa penati baada ya Mchezaji wa Yanga Zawadi Mauya kufanya makosa yaliyozaa Penati,
MCHEZO WA AZIZ KI vs Al Merrikh
▪Ametengeneza nafasi 13
▪Amefunga magoli 3
▪Ame Assist magoli 3