UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, ni muhimu kufanikisha malengo ya kutinga hatua makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo uliopita ugeni, ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba, hivyo Jumapili hii wakiwa wanarudiana, Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote, au sare ya bao 1-1 kushuka chini ili ifuzu.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, ameweka wazi kuwa watatumia Uwanja wa Azam Complex kukamilisha kazi ya kufuzu hatua ya makundi.
“Tunawakabili Power Dynamos Uwanja wa Azam Complex ambao tutautumia kufuzu hatua ya makundi, mechi itakuwa saa 10 jioni kwa kuwa michezo mingi tulicheza kwenye muda huo.
“Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wengi wanaoujua uwanja ule na wengine hawaujui.

