KLABU ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini wametangaza kifo cha Afisa wao mwandamizi Stanley ‘Screamer’ Tshabalala. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Kocha huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana alilazwa hospitali hivi karibuni baada ya kupigwa risasi wakati akiwa katika mapumziko kwenye makazi yake mwezi Machi mwaka huu.
Tshabalala mwenye umri wa miaka 75 alikuwa akiendelea vizuri na matibabu madogo madogo nyumbani kwake lakini baadaye alizidiwa na kukimbizwa hospitali ambapo jana Alhamisi mchana aliaga dunia.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
“Familia ya Tshabalala na Orlando Pirates kwa masikitiko makubwa inatangaza kifo cha mpendwa wetu Stanley Tshabalala mchana wa leo (jana) hospitalini,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.
“Bra Stan, kama alivyotajwa kwa upendo na kila mtu, alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata alipopigwa risasi mwezi Machi mwaka huu.
“Familia ya Tshabalala na Orlando Pirates itatoa taratibu zingine za mazishi na maombolezo ya msiba huo. Tunawaomba umma uwe na subira, tutatoa maelekezo yote kadri mipango inavoendelea.”
Tshabalala, aliyezaliwa mwaka 1949, alikuwa gwiji ndani na nje ya uwanja. Mwanachama na mwanzilishi wa Klabu ambayo ni wapinzani wa Orlando Pirates, Kaizer Chiefs. Pia, aliwahi kufanya kazi kama skauti mkuu wa Kaizer. Mchezaji huyo mzaliwa wa Orlando-Mashariki alipata jina lake la utani wakati akicheza soka.