Lawrence Siphiwe Tshabalala ndie aliyekua kiungo wa kati wa timu ya Afrika ya kusini aliye zaliwa septemba 25 mwaka 1984. Tshabalala amekua ni moja kati ya wachezaji maarufu zaidi nchini Afrika ya Kusini kwa kizazi chake, yeye ndie alikua mchezaji wa kwanza kucheza kimataifa wakati bado anatumikia timu ya taifa, na ndie mchezaji wa pili kwa chi yake aliyehudumu kwa muda mrefu katika timu ya taifa huku akicheza mara tatu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika na pia kushiriki katika kombe la dunia lililofanyika Afrika ya kusini mwaka 2010.
Timu ya Afrika ya kusini haikufanya vema kwenye mashindano hayo kwa mwaka 2010 lakini furaha ya wa Afrika na dunia kiujumla ilikua ni kuona ameibuka mtu mwenye Asili ya Africa anashinda goli katika mashindano hayo.
Kwenye michuano ya kombe la dunia la mwaka 2010 Tshabalala alifunga goli la kwanza la michuano hiyo na kufanya goli hilo lililojulikana kama Goli la maajabu kushindania Tuzo ya FIFA PUSKAS AWARD mwezi August 2015.
Tshabalala alifunga goli mita 40 na kufanya goli hilo kua goli maarufu duniani na kupata zaidi ya watazamaji Milioni 70 ndani ya dakika ya kwanza tangu lirushwe kwenye mtandao nchini Uingeleza.
Tshabalala ni mchezaji wa pembeni kiasili lakini anaweza kucheza kati pia.
Issa
Goli makin