Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuwa hasira zao zote zipo kwenye mchezo wa kesho jumapili dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga waipania Tanzania Prisons

Hiyo inakuja baada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Highland Estates, Mbarali Jijini Mbeya.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema “Maandalizi yetu yamekamilika kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

“Tanzania Prisons ni timu ngumu mara zote ambazo tunakutana nao hivyo tutaingia kwa kuwaheshimu lakini sisi tuna hasira nao kutokana na matokeo tuliyoyapata kwenye mchezo uliopita.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa