Straika wa zamani wa Yanga na Simba ambaye kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Singida Big Stars, Amosi Tambwe ameanza kutupia mabao ndani ya ligi kuu.

Tambwe alikuwa na kikosi hicho msimu uliopita ambapo alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa kikosi hicho kilichokuwa kinashiriki michuano ya Championship.
Nyota huyo alifunga bao jana ijumaa dhidi ya Namungo ambapo Singida Big Stars waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mabao mengine ya Singida yamefungwa na Meddie Kagere na Said Ndemla na kuisaidia timu hiyo kufikisha jumla ya pointi 30.

