Simba Yafunga Barabara Zote Tanga

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake dhidi ya Coastal Union uliopigwa katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Wekundu wa Msimbazi walifanikia kupata ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya Coastal Union na kukusanya alama zote tatu huku wakifikisha jumla ya alama 34 katika michezo 15 ambayo wamecheza mpaka sasa.simbaAlikua ni yuleyule mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba raia nchini Zambia Jenerali Moses Phiri aliyefanikiwa kufunga mabao mawili huku kiungo fundi Clatous Chota Chama akifanikiwa kuhitimisha karamu hiyo baada ya kupigilia msumari wa tatu.

Timu ya Coastal Union maarufu kama wanamangushi baada ya kupoteza leo dhidi ya wekundu wa msimbazi wanakua wamepoteza mchezo wa tano mfululizo kwenye ligi kuu ya NBC msimu huku wakiwa nafasi ya 13 na alama zao 12.simbaKlabu ya Simba leo wamefanikiwa kurudi kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 34 wakiwashusha mabingwa watetezi klabu ya Yanga waliokua na wanaongoza ligi kwa alama 32.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.