Phiri, Mayele Vita Bado Mbichi

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Moses Phiri na Fiston Mayele vita yao kwenye kiatu cha mfungaji bora inaonekana bado mbichi sana kutokana na muenendo wa washambuliaji hao kwenye michezo ya ligi kuu ya NBC.

Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri leo amefanikiwa kufunga magoli mawili kwenye ushindi wa mabao matatu kwa bila walioupata klabu ya Simba huku akifanikiwa kufikisha mabao 10 kwenye ligi kuu ya NBC.phiriBaada ya kufikisha jumla ya mabao 10 mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Zambia anayekipiga katika klabu ya Simba amefanikiwa kumfikia Fiston Mayele ambaye ndio alikua kinara wa mabao akiwa na mabao 10.

Baada ya washambuliaji hao kulingana kwa mabao inaonesha kua vita ya kugombea kiatu hicho bado iko wazi sana kwani Phiri ameshawahi kumpita Mayele na Mayele nae alikuja kupindua meza na kwasasa wako sawa kwa idadi ya mabao.phiriWakati vita ya kugombea kiatu cha mfungaji bora inaendelea kuna vita nyingine inaendelea ya pasi za mwisho ambapo mpka kufikia leo mwamba wa Lusaka Clatous Chama amekaa kileleni akiwa na pasi 7 za mabao akifuatiwa na Ayub Lyanga na Sixtus Sabilo wote wakiwa na pasi 6 za mabao.

Acha ujumbe