Uholanzi Watinga Robo Fainali Kibabe

Timu ya taifa ya Uholanzi chini ya kocha louis Van Gaal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuibamiza timu ya taifa ya Marekani kwenye hatua ya 16 bora mapema leo.

Vijana wa Louis Van Gaal wamefanikiwa kuichakaza timu ya taifa ya Marekani kwa jumla ya mabao matatu kwa moja katika mchezo uliopigwa katika dimba la Khalifa International na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali.uholanziMabao ya Mephis Depay, Daley Blind, pamoja na Denzel Dumfries yalitosha kuwapa Uholanzi ushindi huku bao la kufutia machozi la timu ya taifa ya Marekani likifungwa na Haji Wright na kutupwa nje ya michuano hiyo.

Timu ya taifa ya Uholanzi wanasubiri mshindi wa mchezo wa usiku kati ya timu ya taifa ya Argentina dhidi ya Australia ambapo atakaeshinda hapo anaelekea kumenyana na Uholanzi ambaye tayari ameshafuzu jioni ya leo.uholanziKama itatokea hatua ya Robo fainali watakutana Uholanzi na Argentina basi itakua ni mechi ya kisasi baina ya wababe hao, Kwani Uholanzi watahitaji kulipiza kisasi pale walipotolewa kwenye hatua ya nusu fainali mwaka 2014 Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.