Gwiji wa soka kutoka nchini Brazil Edson Arantes Do Nascimento maarufu kama Pele ameripotiwa kua kwenye hali mbaya kiafya baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ambao umekua ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.
Gwiji huyo ambaye kwasasa inaelezwa hakuna mionzi yeyote ambayo inaweza kumfanya apone kutokana na tatizo la saratani linalomsumbua kwa muda mrefu. Kwasasa gwiji huyo amewekwa kwenye uangalizi maalumu ili kumpunguzia maumivu na pia asipate changaoto ya kupumua.Kwa kawaida ugonjwa wa saratani ukishafika kwenye kiwango cha mwisho hua hakuna tiba ambayo inaweza kumponya mgonjwa zaidi hua ni kutumia dawa za kupunguza maumivu mpaka pale uhai wa mgonjwa utakapofikia tamati. Na hali hii ndiyo anayopitia gwiji Pele kwasasa huku dunia nzima ikimuombea gwiji huyo kwani ni miongoni mwa wachezaji bora wa muda wote ambao dunia imewahi kuwatazama.
Pele ni mchezaji pekee ambaye amewahi kushinda kombe la dunia mara tatu huku akifanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti kwenye mpira wa miguu na wengine huenda mbali zaidi na kumuita mfalme wa mpira wa miguu duniani.Kinachoendelea kwasasa kwa gwiji huyo ni dunia ya wapenda mpira kusimama kwa pamoja na kumuombea mchezaji huyo bora wa muda wote kutokana na tatizo ambalo analipitia kuonekana halina tiba tena.