Klabu ya soka ya Yanga imeendelea kubaki kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kuifunga klabu ya Mbeya City kwa mabao mawili kwa bila katika dimba la Benjamin mkapa jijini Dar-es-salaam.

Yanga walifanikiwa kupata bao katika kila kipindi huku wakitandaza soka safi na kuwasaidia kupata alama tatu muhimu na kufikisha alama 32 kwenye michezo 12 waliyocheza mpaka sasa. Mabao ya Fiston Kalala Mayele ndio yalipeleka kilio kwa klabu ya Mbeya City leo hii.yangaKlabu hiyo ambayo kwasasa inakimbiza kwa rekodi ya kutokufungwa na leo imefanikiwa kufikisha michezo 49 bila kupoteza katika ligi kuu ya NBC. Wakati wananchi wakiwa kileleni kwenye msimamo mshambuliaji wake hatari pia Fiston Mayele nae yupo kileleni kwenye mbio za ufungaji bora baada ya kufikisha mabao 10.

Mayele ambaye amekua kwenye kiwango bora sana alifanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo huo ambayo ndio yaliipa timu hiyo alama tatu muhimu huku yeye akiendelea kuongoza kwenye mbio za Ufungaji huku anaemfutia akiwa na mabao 7 ambaye ni Sixtus Sabilo wa Mbeya City.yangaYanga kwasasa wamefikia rekodi ya klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo ilifanikiwa kucheza michezo 49 ya ligi kuu ya Uingereza bila kupoteza katika msimu wa 2003/2004. Huku kwasasa wakiitafuta rekodi ya Bayern Munich ya michezo 53 bila kupoteza

PAN

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa