Kikosi cha Yanga SC, kikiambata na baadhi ya viongozi kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa makundi ya CAF Champions League dhidi ya CR BELOUIZDAD.

Kikosi kilichoondoka leo alfajiri kimeondoka na nyota baadhi, na nyota wengine ambao wapo timu ya Taifa Stars wanatarajia kuondoka alfajiri ya kesho wakiambatana baadhi ya viongozi akiwemo Makamu wa Rais Yanga SC, Arafat Haji.YANGAYanga SC pia imeshafanya utaratibu mzuri wa wachezaji wake, Khalid Aucho, Stephene Aziz Ki na Djigui Diara ambao wapo pia kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, waungane moja kwa moja na kikosi nchini Algeria mara baada tu ya michezo yao kufuzu kombe la Dunia itakapomalizika.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa