MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Mkapa Dar kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosa Jumamosi ya wiki hii.

Ahmed Ally alisema: “Mchezo huu unahitaji zaidi mashabiki kuja uwanjani, tunataka kuendeleza utamaduni wa kujaza uwanja.

“Tumewachukua mashabiki waje kuwambia mashabiki wenzao kuja uwanjani. Hivi karibuni tumepata tuzo ya mashabiki bora Afrika kama klabu tunataka kuwashukuru kwa kazi kubwa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa