Bruno Fernandes Vitani na Bernardo Silva

Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes ameingia vitani na kiungo mwenzake wa kimataifa wa Ureno ambaye anakipiga klabu ya Man City kwasababu ya kinda ya kireno Joao Neves.

Kiungo Joao Neves amewaingiza vitani viungo Bruno Fernandes na Bernardo Silva, Kwani wote wanapmbana kumshawishi kiungo huyo kinda ajiunge na vilabu vyao.bruno fernandesKiungo Joao Neves mwenye miaka 19 tu amekua akionesha ubora mkubwa akiwa na klabu ya Benfica na timu ya taifa ya Ureno, Huku akitabiriwa makubwa siku za usoni kutokana na ubora wake akiwa kijana mdogo.

Kiungo Bruno Fernandes alikaririwa akisema kiungo huyo ni mchezaji mzuri sana na angetamani ajiunge na Man United, Huku Bernardo nae akisema kiungo Joao Neves ni mchezaji mwenye ubora mkubwa ambaye angekua anafanya maamuzi angetamani ajiunge na Man City.bruno fernandesTaarifa kutoka ndani ya Manchester United zinasema kua klabu hiyo imeshatuma maskauti wake mara kadhaa kumfatilia kiungo huyo kwenye michezo ambayo anaitumikia klabu yake ya Benfica, Hivo Man United mpaka sasa wanaonekana wako hatua moja mbele ya Man City kwa Joao Neves.

Acha ujumbe