Klabu ya Yanga baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc kule mkoani Mbeya wamefanikiwa kurejea katika jia ya ushindi baada ya kuifunga klabu ya Geita Gold kwa mabao matatu kwa bila.
Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi huo wa mabao matatu kwa bila na mpira mkubwa, Hii inaonesha dalili nzuri kwa vijana hao wa kocha Gamondi kuweza kurudi kwenye ubora wao.Wananchi walianza mchezo huo kwa kasi ya juu wakionekana kuutawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa kabisa, Lakini Geita Gold walionekana kukaa nyuma na kuzuia vizuri mpaka ilipofika dakika ya 44 Pacome Zouzoua kufunga bao la kwanza kabla ya Aziz Ki kuweka bao la pili katika dakika ya 45+2 na kuwafanya Wananchi kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili kilianza huku mabingwa hao watetezi wakiendelea walipoishia na kuonesha bado wana njaa ya kuendelea kuongeza mabao kutokana na mashambulizi ambayo walikua wakifanya, Ambapo dakika ya 69 ya mchezo Maxi Mpia Nzengeli aliweka bao la tatu.Klabu ya Yanga sasa wanakua wamefikisha alama 12 katika michezo mitano ambayo tayari wameshaicheza wakifanikiwa kushinda michezo minne mpaka sasa, Huku wakipoteza mchezo mmoja ambao ulikua dhidi ya Ihefu Fc.