YANGA YAMALIZA NA CHIVAVIRO

Taarifa kutoka kwenye moja ya Chanzo chakuaminika kutoka Afrika Kusini Kimethibitisha kuwa, Raisi wa klab ya Yanga Hersi Said amekamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Kati wa klab ya Kaizer Chiefs Ranga Chivaviro (30).

Pia bado haijafahamika vizuri ukubwa wa mkataba wake aliomalizana na Yanga na muda atakao jiunga nao kambini, Ila taarifa za uhakika ni kwamba Ranga Chivaviro ni Mwananchi Mpaka sasa.YANGAFahamu kuwa Rais wa Yanga Eng.Hersi Said yupo Afrika Kusini na alikutana na viongozi wa Kaizer Chiefs na kwenye mkutano huo wakamaliza na jambo la straika huyo wa zamani wa Marumo Gallants.

Ikumbukwe kuwa Chivaviro alikuwa amebakiza hatua chache kwenye usajili wa dirisha dogo na sasa inaonekana kila kitu kipo sawa.

Acha ujumbe