AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI SIMBA

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa na utulivu ili kuwapunguzia presha viongozi wa timu hiyo ili wasifanye maamuzi ambayo sio sahihi kwa timu hiyo ambayo yanaweza kupelekea kufanya vibaya.

Ahmed Ally alisema huu ni muda ambao wanatakiwa kuwa pamoja na kuipambania timu yao ili iweze kufikia malengo, lakini kubwa kuwapa moyo viongozi wao kwenye wakati huu mgumu.AHMED ALLY“Tuwamini viongozi wetu, tukikubali kuchanganyikiwa sasa hata mzunguko wa kwanza bado haujaisha tutapotea sana.

“Timu yetu bado inatakiwa kucheza mechi za ligi zilizosalia na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa,” alisema Ahmed Ally.

Acha ujumbe