Napoli Waondoka na Mikeka

Klabu ya Napoli imechana kwelikweli hiyo ni baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila mbele ya klabu ya Empoli katika mchezo wa ligi kuu ya Italia uliopigwa mchana huu.

Napoli ambao walionekana muda mwingi kuukamata mchezo lakini mambo hayakua mambo mwishoni mwa mchezo kwani ni Empoli ambao walifanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu.napoliMabingwa hao watetezi wa soka nchini Italia wamekua hawana msimu mzuri sana tangu kuondoka kwa kocha wao Luciano Spalletti ambaye amejiunga na timu ya taifa ya Italia.

Klabu hiyo mpaka sasa wameshapoteza michezo mitatu na kusare michezo mitatu jambo ambalo msimu uliomalizika mpaka wakati huu hawakua wamepoteza mchezo hata mmoja hii inaonesha  fomu yao ipo chini.Napoli wamepoteza mchezo huo baada ya kumiliki mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini Empoli wao walipata bao lao dakika ya 90 ya mchezo, Ambapo halikutoa fursa kwa klabu hiyo kuweza kusawazisha bao hilo na kumaliza mchezo kwa kipigo wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

Acha ujumbe