Klabu ya Yanga nao wakaona wasifunge dirisha la usajili bila kusajili golikipa na sasa wamehamia kwa aliyekuwa golikipa wao wa zamani Metacha Mnata ambaye ni mlinda mlango nambari 1 wa Singida Big Stars kwa mkopo wa miezi 6.

Yanga wamemrudisha Metacha ambaye aliwahi kucheza klabuni hapo kabla ya kuondoka na kuitumikia Polisi Tanzania ambayo bado ina hali mbaya kwenye msimamo wa ligi ambapo ipo nafasi ya mwisho.
Baada ya hapo Metacha alijiunga na Singida Big Stars ya Pluijm ambayo imepanda daraja msimu huu na inafanya vizuri.

Nabi na timu yake wameamua kumchukua Metacha kwani ana uzoefu na timu hiyo lakini pia kutokana na Mshery ambae ni golikipa namba mbili kupata majeraha. Na aliyebaki ni Diara na Johora kiwango chake hakiridhishi.

