Yanga Yapangwa na Rivers United Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho

Klabu nyingine inayoshirikishi michuano ya CAF ni klabu ya Yanga ambayo inaongozwa na kocha mkuu Nasredine Nabbi kwa upande wao wanashiriki Kombe la Shirikisho na wamepangwa na Rivers United kutoka Nigeria.

 

Yanga Yapangwa na Rivers United Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho

Yanga ilimaliza kinara wa kundi D akiwa na pointi 13 baada ya kumfunga nje ndani TP Mazembe na kupangiwa na Rivers ambaye alikutana naye mwaka jana kwenye hatua za awali kwenye michuano ya klabu bingwa na akatolewa.

Sasa ni Young Africans na Rivers tena ambapo vijana wa Nabbi watataka kulipiza kisasi mbele ya timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi ya NPFL wapo nafasi ya pili kwenye kundi B wakiwa na pointi zao 19, baada ya michezo 10, ushindi mara 5, sare 4, kupoteza mara 1.

Yanga Yapangwa na Rivers United Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho

Wakati Yanga wao hapa kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara ndiye vinara wa ligi wakiwa na pointi zao 65, baada ya michezo 24, ushindi mara 21, sare 2, na kupoteza mara 1. Je watafanya nini mbele ya Rivers?

Mechi za mkondo wa kwanza Kombe la Shirikisho zitaanza tarehe 21-23 Nigeria mwezi April na mechi za mkondo wa pili zitaanza tarehe 28-30 Tanzania mwezi April.

Acha ujumbe