Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC klabu ya Yanga wamerejea kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kupata matokeo ya ushindi dhidi klabu ya Namungo mchezo ulipigwa mkoani Lindi.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Ruangwa klabu ya Namungo wakiwa nyumbani wamekubali kipigo cha mabao matatu kwa moja, Huku wakiwaacha mabingwa watetezi wakirejea kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC kwa staili ya namna yake.Mchezo huo ulianza kama kawaida Wananchi wakionekana kuuhitaji mchezo huo kutokana na mashambulizi ambayo walikua wakiyafanya katika lango la Namungo, Lakini wauaji hao wa kusini walifanikiwa kuzuia kwa umakini na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi mabingwa hao watetezi wakiendelea kulisakama lango la Namungo, Hakua mwingine ni yuleyule ambaye amekua akiwainua Wananchi kwenye nyakati ngumu Mudathir Yahya aliwapa uongozi Wananchi kabla ya Clement Mzize kuweka kambani bao la pili.
Mchezo uliendelea kwa klabu ya Yanga wakionekana kuhitaji mabao zaidi ambapo kiungo Stephan Aziz Ki akiweka msumari wa tatu, Huku Namungo wakipata bao la kufutia machozi kupitia bao la kujifunga la beki Ibrahim Bacca.Wananchi wanarejea kileleni wakifikisha alama 46 wakiwa na michezo mitatu mkononi Azam Fc wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 44, Huku klabu ya Simba wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama 36 wakiwa na michezo minne mkononi.