Vita ya nafasi nne za juu ligi kuu ya Uingereza inaendelea kupamba moto vibaya sana ambapo klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kuisambaratisha klabu ya Aston Villa leo kwa mabao manne kwa bila.
Tottenham ambao walikua ugenini katika dimba la Villa Park walifanikiwa kupata ushindi mnono katika mchezo mgumu dhidi ya klabu ya Aston Villa ambao wako kwenye kiwango bora kwasasa.Mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kuonekana kuuhitaji mchezo na kushambuliana kwa zamu, Huku Aston Villa wakionekana kupoteza nafasi za wazi kipindi cha kwanza jambo ambalo lilifanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo ni vijana wa kocha Ange waliofanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa James Maddison dakika ya 50 ya mchezo kabla ya kijana Brennan Johnson kuongeza bao la pili kwa Spurs dakika ya tatu baadae.
Aston Villa wakijitahidi kupata bao la kusawazisa ndipo kiungo wake McGinn alipocheza faulo ya hatari mnamo dakika ya 65 na kupelekea kuonyeshwa kadi nyekundu, Huku akiwaacha wenzake na mzigo mzito sana.Nahodha Heung Ming Son alifunga goli la tatu dakika 91 ya nmyongeza huku Timo Werner aliyetokea nje akipiga msumari wa mwisho dakika ya 94, Ambapo sasa Tottenham wanafikisha alama 53 katika nafasi ya tano huku Aston Villa wakiwa nafasi ya nne na alama zao 55 wakati huo Spurs wakiwa na mchezo mkononi hii inaonesha kwa namna gani vita ya nafasi ya nne imepamba moto.