YANGA YAWAFUATA MEDEAMA KIBABE

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, leo Desemba 5 alfajiri kimeanza safari kuelekea Ghana kwa ajili ya kupambania kupata pointi tatu muhimu.
Baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imekusanya pointi moja pekee.

Yanga inapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Medeama Desemba 8.yangaMiongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Hafiz Konkoni, Mudathiri Yahya, Skudu Makudubela.

Ikumbukwe kwamba Yanga Desemba 2 ilishuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Al Ahly baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga 1-1 Al Ahly.yangaBao la Pacome Zouzoa dakika ya 90 limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Acha ujumbe