Nimelitazama sakata la Ibrahim Ajibu, inasemekana kuna baadhi ya watu wanataka arejee Yanga ila asilimia kubwa hawamtaki

Kutomtaka sio kwamba hana ubora, sio kwamba hawezi kucheza Yanga ila ni matokeo ya namna ya uondokaji wake au matendo yake

Ajibu akanikumbusha kisa kimoja kati ya FC Barcelona na Mchezaji anaitwa Sergi Guardiola, waliemsajili December 2015

Walimsajili Guardiola kwenye timu yao ya akiba, lakini baadae wakaanza kupitia posts kwenye mitandao yake ya kijamii, kuona utashi wake upoje

Ajibu

Sergi Guardiola miaka kadhaa nyuma aliandika vitu vingi kuikosoa Barcelona, aliandika vingi kuikosoa Catalunya kama Jimbo na mwisho alikuwa na Jumbe za kuisifia Real Madrid

Kwa haraka sana Barcelona wakavunja nae mkataba, kutokana na matokeo ya vitendo vyake mwenyewe Sergi Guardiola, ukawa mkataba mfupi zaidi kuwahi kusainiwa na kuvunjwa

Mchukue Ajibu na Sergi Guardiola hata kwenye maisha ya kawaida, usipende sana kumaliza maneno


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa