Kocha wa sasa wa As Roma, Jose Mourinho amemfananisha mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish na nguli wa soka wa zamani legendari Luis Figo.

Zikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya michuano ya EURO 2020 kuanza rasmi, Mourinho ametaja kikosi chake ambacho angepanga kwa upande wa England kama angekuwa kocha.

Katika majina aliyotaja, Mourinho alionekana kumkubali sana Grealish huku akimfananisha na Luis Figo kwenye ubora wake wa kufungua nafasi na kujiwekea maeneo hatari kwa mpinzani awapo Uwanjani.

Mourinho alimuelezea Grealish kama mchezaji machachari na hatari sana akikata ndani kutoka kushoto huku akiwa mtu asiyeshikika na mabeki wa timu pinzani.

Katika kikosi hicho Mourinho alimtaja mchezaji mmoja tu kutoka United, ambaye ni Kipa Dean Henderson huku Rashford na Luke Shaw wakiachwa nje, Mourinho akidai hawajamshangaza sana msimu huu.

Kikosi kamili ambacho Mourinho anadai angekipanga dhidi ya Croatia jumapili hii ni Dean Henderson (kipa), mabeki wanne John Stones, Tyrone Mings, Ben Chilwell na Kyle Walker.

Viungo wa chini wakiwa ni Declan Rice na Kelvin Philips,na mbele wakiwa ni Grealish, Mason Mount, Foden na Kane kama straika pekee.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa