Wijnaldum akiwa benchi na mchezo unaendelea Akaumia Robertson mapema sana lakini Captain Hendo alimfuata na kumuambia, ‘Endelea kukaza, wewe ni Scouser’. Kama hufahamu Scouser ni mtu anayetokea Merseyside Liverpool.

Kumbuka Liverpool alikuwa na mlima wa kupanda baada ya kufa tatu bila kule Catalunya katika mechi ya kwanza, tena mlima walitakiwa wapande bila washambuliaji wawili hatari zaidi England, Mo Salah na Bobby Firmino.

Wijnaldum
Wijnaldum

Baada ya Robertson kushindwa kuendelea Klopp alimnyanyua Wijnaldum na kumuambia, “Kila mtu anajua namuingiza kiungo wa katikati lakini mimi namuingiza mshambuliaji. Namba tisa wangu Nenda ukanipe mabao”

Hakuna mtu aliyeelewa ile sub, si Kopits zaidi ya elfu hamsini waliokuwa wanawasha moto ndani ya Anfield. Hata kocha msaidizi Peter Krawietz anakiri hakuelewa ile sub kitaalam.

Lakini Klopp anamjua Gini ni mchezaji mtiifu anayemuamini mwalimu wake. Benchi alikuwepo Danny Sturidge ambaye angeweza kucheza ile nafasi kwa asili lakini yeye alimuamini Gini.

Wijnaldum
Wijnaldum

Aliingia Gini na kwenda kutimiza yale maajabu ya Anfield. Kilichofuata ni stori tu. Alirejea kambani mara mbili ndani ya dakika mbili na kazi iliishia pale. Liverpool hao fainali.

Leo Gini anaondoka Liverpool lakini alama yake inabaki pale Anfield milele. Usiku ule dhidi ya Barcelona unabaki vichwani mwa mashabiki wa Liverpool milele.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa