Al Nassr Waachana na Kocha Garcia

Klabu ya Al Nassr kutoka nchini Saudia Arabia imeachana na kocha wake Rudi Garcia mapema leo Alhamisi na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa kimataifa kutoka Croatia Dinko Jelicic.

Taarifa zinaeleza kocha Rudi Garcia ameondolewa na klabu hiyo kutokana na muenendo wa klabu hiyo mpaka sasa ambapo inaelezwa haujawaridhisha mabosi wa timu, Huku kubwa zaidi ni kupoteza nafasi ya uongozi katika msimamo wa ligi kuu ya Saudia Arabia ambapo walikua wakiongoza.Al NassrKlabu hiyo ambayo nyota wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Man United, na Juventus Cristiano Ronaldo anaitumikia kwasasa imeachana na kocha huyo kwa makubaliano yua pande zote, Lakini kabla ya timu kuchukuliwa na Dinko Jelicic kocha Jose Mourinho alikua anahusishwa kuchukua timu hiyo.

Kocha Jelicic raia wa kimataifa wa Croatia amepewa nafasi ya kuinoa timu ya Al Nassr akitokea timu hiyo ya vijana chini ya miaka 19, Hivo ni kama kocha huyo amepandishwa wadhifa kutoka kuinoa timu ya vijana mpaka kupewa timu kubwa yenye nyota wakubwa kama Cristiano Ronaldo.Al NassrKwakua klabu ya Al Nassr wameachana na Mfaransa Rudi Garcia kwa makubaliano ya pande zote mbili na kumtakia kila kheri kwenye safari yake ya kisoka hiyo ni kupitia taarifa ya klabu hiyo, Rudi Garcia amewahi kuvifundisha vilabu vya Olympique Marseille,Lyon, As Roma, lakini pia akiiongoza Lille kutwaa ubingwa wa Ligue 1 mwaka 2011.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.