ALI Kamwe ambaye Ofisa Habari wa Yanga amepelekwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, (TFF) na Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Masanzala.
Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB), imeeleza kuwa katika kikoa cha Februari 12 2025 walipitia mwenendo wa matukio ya ligi na kutoa angalizo kwa timu kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani wakati wa mechi ikitokea uwanja utafungwa.
Hiyo imetokana na mechi namba 139 Pamba Jiji 1-0 Azam FC, Klabu ya Pamba Jiji kutozwa faini ya milioni mbili kwa kosa la mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea mara baada ya mchezo kumalizika.
Kitendo cha mashabiki hao kuingia kiwanjani kilisababisha kuvunjika mahojiano ya makocha yaliyokuwa yakifanywa na mdhamini mwenye haki ya matangazo ya runinga,Azam TV.