Manchester United wanaripotiwa kufikiria kumuacha Amad Diallo aondoke kwa mkopo wakati wa kampeni ya 2021-22.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 aliwasili rasmi Old Trafford kutoka Atalanta BC mnamo Januari na akaonekana mara nane kwenye mechi za Mashetani Wekundu katika nusu ya pili ya kampeni ya 2020-21, akifunga mara moja na kutoa asisti 1.
Kwa mujibu wa ESPN, Amad atakuwa sehemu ya maandalizi ya msimu wa mapema wa Man United, ambao unaanza baada ya mwezi ujao. Kabla ya uamuzi kutolewa kama uhamisho wa mkopo utakuwa wa faida katika hatua hii ya taaluma yake.

Ripoti hiyo inadai kwamba Mashetani Wekundu pia wanaweza kuwaruhusu James Garner, Shola Shoretire, Anthony Elanga na Hannibal Mejbri kuondoka.
Amad alishiriki katika mechi tatu za mwisho za Man United za msimu wa Ligi ya Premier ya 2020-21, lakini alikuwa mbadala asiyetumiwa wa fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Villarreal.
Kuwasili kwa Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund kwa dau la pauni milioni 80 kunaweza kuathiri mda wa kucheza wa kijana huyo muhula ujao.


