Amin Mohamed Omar ni mwamuzi maarufu kutoka Misri ambaye kwa sasa anatajwa kuwa miongoni mwa waamuzi bora barani Afrika. Alizaliwa Septemba 25, 1985, katika eneo la Mohandseen jijini Cairo, Misri. Safari yake ya uamuzi ilianza rasmi mwaka 2013 akiwa kwenye Ligi Kuu ya nchini kwao, na kufikia mwaka 2017 alipata beji ya FIFA ambayo ilimfungulia milango ya kimataifa. Tangu hapo, Amin ameendelea kujizolea sifa kwa msimamo wake thabiti na uaminifu kazini, jambo ambalo limewavutia wengi kwenye tasnia ya soka la Afrika.
Hivi karibuni, Amin alikuwa mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mechi ya Stellenbosch dhidi ya Simba SC kule Afrika Kusini, lakini alilazimika kubadilishwa dakika za mwisho kutokana na majeraha. Hii si mara ya kwanza kwa Amin Omar kuhusika kwenye michezo mikubwa yenye presha. Aliwahi kuchezesha nusu fainali ya AFCON mwaka jana kati ya Nigeria na Afrika Kusini, ambapo alitoa kadi nyekundu kwa Grant Kekana, uamuzi ulioleta mijadala mikubwa.
Katika kumbukumbu nyingine, Amin amechezesha mechi ya ufunguzi ya AFCON kati ya Ivory Coast na Guinea Bissau, na pia alikuwepo kwenye Kombe la Dunia la U-17 lililofanyika Brazil mwaka 2019. Kwa upande wa vilabu vya Afrika, Omar ameshaiongoza Simba SC kwenye mechi dhidi ya Horoya mwezi Novemba 2023, ambapo Simba walipoteza kwa bao 1-0 katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Vilevile, ameshaichezesha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya DR Congo katika mechi ya AFCON iliyomalizika bila kufungana.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa ujumla, Amin Mohamed Omar ameshachezesha michezo 17 ya CAF kwa upande wa vilabu na sita kwa timu za taifa. Katika mechi hizo, ametoa jumla ya kadi 13 za njano, tatu nyekundu na mikwaju mitatu ya penalti. Nyumbani kwao Misri, amewahi kuaminiwa kuongoza mechi yenye ushindani mkubwa Zaidi, Al Ahly dhidi ya Zamalek kwenye fainali ya Egypt Super Cup, mchezo unaotajwa kuwa na presha kubwa zaidi hata kuliko derby ya Simba na Yanga.
Mijadala imeibuka ya kwa nini waamuzi wa aina hii hawachezeshi mara nyingi nyumbani kwao? Sababu kuu ni imani ya muda mrefu nchini Misri kwamba familia za waamuzi huwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya vilabu, jambo linalozua hofu ya upendeleo. Hivyo, wanapopelekwa kwenye mechi zisizohusiana na klabu hizo kama vile Yanga dhidi ya Simba, wanakuwa na fursa ya kutoa maamuzi ya haki na yasiyoegemea upande wowote.
Kikatiba, hakuna zuio katika kanuni za Ligi Kuu ya Tanzania linalokataza matumizi ya waamuzi kutoka nje ya nchi. Hali hii imeacha mwanya wa kutumia wataalamu wa kimataifa kama Amin, hasa kwenye michezo mikubwa kama Yanga dhidi ya Simba. Japokuwa ni mtu mpole nje ya uwanja, ndani ya uwanja ni mtu mkali na mwenye maamuzi magumu sana.