Habari kutoka Yanga, zinasema tayari mabosi wa klabu hiyo wameanzisha mazungumzo na FAR Rabat ya Morocco ili kuona kama kuna uwezekano wa kuipata saini ya beki Inonga Bakka.

Na hiyo ni kwa vile bado ana mkataba wa Mwaka mmoja na kikosi hicho kilichomsajili mwanzoni mwa msimu huu kutoka Simba.
Beki huyo wa kimataifa wa DR Congo, anapigiwa hesabu za kutua Yanga kuongeza nguvu eneo la ulinzi la kati linaloongozwa na Dickson Job na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Bakari Mwamnyeto ambaye amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza.
Chanzo cha habari Hii kilisema: “Yanga ina uhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo. Ila kuhusu nani anakuja ni mapema kuzungumza kwa sasa, lakini mchakato unaendelea na majina ya wachezaji wanaotazamwa kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo hilo yapo mezani na tayari yameanza kufanyiwa mchakato na jina la Inonga ni miongoni mwao,”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Chanzo hicho kiliongeza kuwa mchakato wa kutafutwa kwa beki huyo ulianza baada ya kuachana na Gift Fred kutoka Uganda na tangu hapo Yanga wamekuwa na wakati mgumu kupata mchezaji ambaye ataweza kuendana na ushindani uliopo hasa kwenye eneo hilo.

Inonga amekuwa beki tegemeo kwa sasa wa kikosi cha AS FAR Rabat, kilichoondolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya awali kufungwa 4-1 ugenini na kuja kushinda nyumbani mabao 2-0.

