Amrabat Ndoto imetimia

Wakala wa mchezaji mpya wa Manchester United Sofyan Amrabat kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameeleza kiungo huyo kujiunga na Man United ni ndoto iliyotimia.

Wakala wa Amrabat ameeleza mchezaji huyo alikataa kila klabu ambayo ilikua inamuhitaji katika dirisha kubwa la usajili lililopita, Huku matumaini yake yakiwa ni kucheza klabu ya Manchester United ambayo ilikua ni klabu ya ndoto yake.AMRABATWakala wa kiungo huyo ameeleza wazi wamepitia changamoto nyingi katika miezi mitatu iliyopita juu ya sakata la yeye kutimka klabu ya Fiorentina, Lakini wanamshukuru Mungu kwakua wamefanikiwa kukamilisha ndoto hiyo.

Wakala huyo pia akimshukuru kiungo Amrabat kwa kumuamini kwa kipindi chote cha takribani miaka 15 na kumfanya yeye kua moja ya watu walifanikisha ndoto ya kiungo huyo kukipiga katika dimba la Old Trafford kama mchezaji wa Man United kutimia.AMRABATManchester United walikamilisha usajili wa fundi huyo siku ya mwisho ya usajili kwa mkopo wa msimu mzima, Huku ikielezwa Man United wana uwezo wa kumsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco.

Acha ujumbe