Kocha wa Arsenal, Unai Emery amewataka Arsenal kuendelea kukaza mechi zake zilizosalia msimu huu na kwamba kwa hatua iliyopo kila mechi kwao ni kama fainali. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia juu ya uwezekano wa wao kukaa kileleni na kuendelea kuikamata nafasi hiyo ya juu ya ligi. Na kwa hali hiyo amewasihi kufanya vyema zaidi kwenye mechi yao ya Jumapili mbele ya Everton.
Kukaa nafasi nne za juu kwenye ligi ambayo ushindani wake sio wa kawaida ni jambo linalohitaji nguvu kwa kiwango fulani na utimamu wa wachezajj tegemezi wanaopatikana kwenye kikosi husika kwa wakati huo. Amewataka wachezaji kupigana kwa kila namna kuhakikisha hawaachii alama yoyote ile kwa mechi hizi.
Arsenal walipanda hadi nafasi ya tatu kwa mara ya kwanza msimu huu huku wakiwa wanasubiri mtanange kati ya Tottenham na Newcastle kitu ambacho hakikudumu hata kwa masaa 48 baada ya ushindi huo wakalazimika kushuka tena hadi nafasi ya nne ya ligi hiyo. Japo bado kuna changamoto kuwa kwenye nafasi hiyo.
Upande huo wa Emery bado una nafasi ya kufanya vizuri kwenye nafasi nne za juu na kiuhalisia suala hilo lipo mikononi mwao kama wanahitaji kupanda juu au kushuka kwenye nafasi hiyo. Lakini bado kuna ugumu kwao kutokana na tofauti yao ya magoli iliyopo kati yao na Chelsea na ile ya alama mbili na Manchester United.
Mechi yao dhidi ya Everton sio nyepesi kwa upande wao na wanahitaji jitihada sana kuweza kubadili hali hiyo ili wajilinde zaidi kwenye nafasi hiyo. Everton anakuwa na wakati mzuri kwenye mechi zake nyingi anapokuwa nyumbani na hawi mwepesi wa kuruhusu magoli mepesi kwenye mechi zake nyingi. Kocha bado ana matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zao zilizobaki. Kiuhalisia wana gurudumu zito kulisongesha.
Kikubwa kwenye ligi hiyo kwa sasa ni kuhakikisha wanashinda mechi zilizosalia. Mechi zao nyingi zilizosalia zinachezwa nje na kwamba unakuwa hujiamini. Katika mechi zao zilizopita wamefanikiwa kuondoka na alama tatu.


Furahav
Wapambane sana.
Povel
Wapambene watafikah malengo